Wanafunzi 12,225 waliofaulu mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi na kuingia kidato cha kwanza katika mkoa wa Dar es Salaam wameikosa fursa hiyo kutokana na ukosefu wa madarasa katika mkoa huo.

Hayo yameelezwa jana na Naibu Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo alipokuwa akitoa taarifa kuhusu matokeo ya mtihani wa kumaliza shule ya msingi na kujiunga na kidato cha kwanza nchini.

Naibu Waziri huyo alieleza kuwa wanafunzi 518,034 wamefaulu mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka huu lakini ni wanafunzi 503,914 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za serikali nchini idadi ambayo ni sawa na asilimi 97.3.

Alisema kuwa jumla ya wanafunzi 12,847 wameshindwa kujiunga na kidato cha kwanza nchini kutokana na ukosefu wa madarasa. Idadi hiyo inatokana na wanafunzi 183 katika mkoa wa Dodoma na wanafunzi 200 katika mkoa wa Mtwara.

Jafo alieleza kuwa ili kufanikisha utoaji wa elimu bure hadi kidato cha nne, serikali imetenga shilingi bilioni 131 katika kipindi cha miezi saba.

Dk. Kigwangalla Aweka Mtego Kuwanasa Wachelewaji Wizara ya Afya
Uchaguzi Zanzibar: Jaji Bomani Amshangaa Jecha