Serikali ya Ukraine na waasi wanaotaka kujitenga mashariki mwa nchi ambao wanaoungwa mkono na Urusi wameanza kubadilishana wafungwa.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na wa Ukraine Volodymyr Zelensky kukutana kwa mazungumzo ya ana kwa ana kwa mara ya kwanza mjini Paris mnamo Desemba 9.

Hata hivyo Viongozi hao walikubaliana kuchukua hatua za kusitisha vita pekee vinavyoendelea barani Ulaya kwa sasa.

Mwakilishi wa waasi wa mji wa mashariki mwa Ukraine wa Donetsk, Daria Morozova, amesema kuwa kwa upande wa uasi utarejeshewa wafungwa 87, na wataikabidhi serikali watu wake 55.

Mahusiano kati ya Ukraine na Urusi yaliharibika tangu 2014, Urusi ilipoinyakuwa Rasi ya Crimea na kuwasaidia Waasi wa Maashariki mwa Ukraine kuanzisha vuguvugu la kutaka kujitenga.

Sita wapoteza maisha ajalini Dodoma
Video: Polisi wa kike marufuku kusuka mitindo ya nywele