Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko ameiomba Nato kutuma meli kwenda bahari ya Azov ili kuingilia kati mgogoro wake na Urusi baharini katika eneo la Crimea.

Poroshenko aliliambia gazeti la Ujerumani Bild kuwa anaamini kuwa meli hizo zitapelekwa kuisaidia Ukraine na kuweka ulinzi katika eneo hilo.

Aidha, siku ya Jumapili Urusi ilivamia meli tatu za Ukraine na kuwashika mabaharia wake waliokuwa wakiziongoza kutoka Kerch strait.

Kwa upande wake, Rais wa Urusi Vladimir Putin alimlaumu Rais Poroshenko kwa kuanzisha uhasama wa baharini ili kujiongezea umaarufu kabla ya uchaguzi wa mwaka 2019.

Hata hivyo, siku ya Jumatano umoja wa ulaya (EU) ulilaani vikali vitendo vya Urusi lakini ikashindwa kukubaliana na vikwazo vipya dhidi ya nchi hiyo, huku ikitoa wito kwa Urusi kuziachia meli hizo na mabaharia wake na kuheshimu uhuru wa Ukraine.

 

Waziri Ikupa aagiza walemavu wapewe ajira
Abdelkarim Hassan mchezaji bora Asia 2018