Wakazi wawili wa kata ya Bangwe manispaa ya Kigoma Ujiji wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta kutokana na mvua iliyonyesha kwa saa tano mkoani hapo.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani kigoma ACP Alchelaus Mutalemwa amesema kuwa tukio hilo limetokea februali 25 mwaka huu majira ya saa kumi jioni baada ya ya wakazi hao kuangukiwa na ukuta wa fensi ya nyumba waliyokuwa wamelala.

Amewataja marehemu hao kuwa ni Fatuma Hamisi (38) na mtoto Zainabu Khatibu mwenye mika mitatu ambao ni mama na mtoto wake.

” Ukuta uliowaangukia ulikuwa umelowa kutokana na mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha na baada ya jeshi la Polisi kufika eneo la tukio miili ya marehemu ilichukuliwa na kupelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya Maweni” Amesema ACP Mutalemwa.

Meya wa manispaa ya Kigoma ujiji Hussen Ruhava alifika eneo la tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi kuwa waangalifu wakati mvua zikiendela kunyesha.

“Unajua nyumba yako ina nyufa au imeinama kama ilivyokawaida ya nyumba zetu nyingi, ukiona mvua inanyesha ya upeppo ni vyema ukachukua tahadhari kwa kutoka nje ili ikitokea nyumba ikaanguka muwe salama” Amesema Ruhava.

Saratani ya matiti yawa tishio nchini
Video: Sugu arusha kombora, Kirusi corona kilivyotibua biashara Kariakoo