Jana dunia ilipatwa na kigugumizi baada ya kusambaa kwa kiwango kikubwa taarifa zilizoeleza kuwa tajiri wa dawa za kulevya nchini Mexico, Joaquín Guzmán maarufu kama El Chapo ametoroka gerezani kwa mara ya tatu.

Taarifa hizo zilipata umaarufu mkubwa na kusambazwa kwenye vyombo vya habari vingi huku watumiaji wa mitandao ya kijamii wakitoa picha na ‘meme’ zenye utani kuhusu namna ambavyo El Chapo hawezekani kukaa nyuma ya nondo.

El Chapo Meme

Hata hivyo, ripoti ya kuaminika kutoka nchini Mexico leo imeripotiwa na BBC imeeleza kuwa El Chapo bado anashikiliwa ndani ya gereza lenye ulinzi mkali nchini humo, na hakukuwa hata na dalili za njama za kutoroka.

El Chapo mwenye utajiri wa zaidi ya $1.4 billion amewahi kutoroka mara mbili kutoka katika magereza yenye ulinzi mkali na kamera kila kona nchini Mexico.

Serikali ya Mexico iliahidi kuwa itahakikisha El Chapo ambaye anamtandao mkubwa wa dawa za kulevya hatatoroka tena.

Polisi Watano wauawa katika maandamano ya kupinga mauaji ya Weusi Marekani
Campus Vibez ya Times Fm kuwakutanisha vijana na Naibu Waziri Mavunde kesho asubuhi, Protea hotel