Baada ya heka heka zilizosambaa Afrika mashariki kuhusu Harmonize kukamatwa na Polisi nchini Kenya, hatimaye Harmonize amethibitisha kumaliza tofauti zake na kila aliyekuwa na tatizo naye

Harmonize ameweka wazi kuwa yeye na mchekeshaji Eric Omondi hawana utofauti wowote kama ilivyoripotiwa hapo awali, ambapo Omondi alieneza taarifa kuwa amefanyiwa fujo na kupigwa na msanii huyo.

“Eric ni kaka yangu na ninampenda ni kati ya watu ambao wamekuwa wakichangia kuisukuma tasnia, mimi kabla hata sijawa Harmonize, nimekuwa nikimuona akifanya hizo kazi, kwa hiyo sasa kwenye kilichotokea mimi nilimchukulia kama kaka tu.” amesema Konde Boy.

“Bado sisi ni ndugu na nampenda na kumuheshimu, hakuna aliyekamilika hapa duniani, niko poa kutoka moyoni na kilichotokea kwangu ni kama changamoto za kazi. Na duniani huwezi furahi kila siku, sisi ni ndugu, kitu kimoja, lets go Mombasa i just landed see you tonight.” aliongeza kupitia kwenye Insta story yake.

Baadae Harmonize alishiriki chapisho kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuwa yuko tayari kwa ajili ya onyesho linalofuata ambalo alilifanya jana, usiku wa kuamkia leo Mei 2, 2022, Volume Club huko Mombasa.

Eric Omond yeye ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuweka kipande cha video kikiwaonyesha wawili hao wakiwa ndani ya ndege, punde baada ya kuenea kwa taarifa za wawili hao kugombana.

Katika video hiyo alisikika akimnadi Harmonize kuelekea onyesho lake na kwa uchache akiwaomba radhi Mashabiki walioshitushwa na sintofahamu iliyojitokeza kote mitanaoni kuhusu wawili hao.

Muda mfupi baada ya Konde Boy kukamilisha onyesho lake huko Mombasa, ameitumia Insta story yake kuwataarifu mashabiki zake kuwa yuko mbioni kuachia album mpya ifikapo Mei 20, 2022.

Muongozaji filamu ya Royal Tour awapa 'Neno Zito' wasanii wa Bongo Movie
Pete Davidson avunja ukimya wa mahusiano yake na Kanye West