Uongozi wa klabu ya Mbeya City FC umesema kwamba kwa sasa hawajapokea taarifa zozote kutoka kwa kocha mkuu wa klabu hiyo Kinnah Phiri juu ya swala la kumuhitaji mchezji Mrisho Khalfan Ngasa.

Msemaji wa timu hiyo, Dismasi Teni amesema kwamba kwa sasa uongozi hauwezi kuzungumzia jambo hilo kwakua halipo katika mipango yao bali kilichopo kwa sasa ni juu ya maandalizi ya mchezo wao ujao dhidi ya Azam FC.

“Kwanza nashangaa hizo habari za kusema kuwa kocha mkuu anamuhitaji Ngasa sijui zimetoka wapi maana sisi leo ndio tumerejea kutoka jijini Mwanza na hakuna taarifa zozote juu ya swala hilo”alisema Dismas Teni.

Amesema kwamba kikosi cha timu hiyo tayari kimesharejea jijini Mbeya na siku ya kesho kinataraji kuanza rasmi maandalizi ya mechi hiyo ili wafanikiwe kupata matokeo mazuri yatakayoendelea kuwaweka kwenye nafasi ya kwanza ya msimu wa ligi kuu ya Tanzania bara.

 

Wizara Ya Habari, Utamaduni, Sanaa Na Michezo Kuunda Sera Mpya Ya Sanaa
Serengeti Boys Yaenda Shelisheli