Mtaalamu wa lishe kutoka hospitali ya Taifa Muhumbili, Brenda Maro, amesema kuwa watu wenye mazoea ya kula kupita kiasi wapo katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa saratani.

Amesema ulaji wa kupitiliza, hasa wa vyakula vyenye mafuta na kemikali kwa kiasi kikubwa ndio unaochangia mtu kupata saratani.

“Mazoea ya kula kupita kiasi yanaweza kupelekea uzito mkubwa baadaye, hasa sehemu kubwa ya vyakula ikiwa na vya mafuta mengi, vyakula vya kusindikwa na aina mbalimbali za kemikali ni moja ya hatari ya maradhi kama vile saratani”

” Ila pia eneo kubwa ikiwa ni wanga, mtu ‘ana – overwork’ kongosho ambalo kazi yake kubwa ni kuachilia ‘ insulini’ inayotumika kupeleka ‘ glucose’ kwenye ‘cell’ hivyo kupelekea kulichosha.

” kongosho huwa ina kazi kubwa ya ‘ku control blood sugar’ kwahiyo ikiwa haifanyi kazi yake ipasavyo sukari hubaki nyingi katika damu” amefafanua Dkt. Brenda alipo ongea na Mtanzania.

Daktari bingwa wa magonjwa ya saratani kutoka taasisi ya saratani ya Ocean Road, Dkt. Hellen Makwani ameeleza kuwa mtu akiwa na uzito mkubwa mara nyingi ni rahisi kupata saratani ya kongosho na saratani ya utumbo.

Mwinyi Zahera: Nipo tayari kwa lolote Yanga
Spurs, Ufaransa kumkosa Hugo Lloris hadi 2020