Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, amewaagiza Maafisa uvuvi kuweka hadharani tozo za samaki pamoja na mazao ya uvuvi kwa wafanyabiashara wa bidhaa hizo.

Ametoa agizo hilo katika soko la samaki la kimataifa la Kirumba jijini Mwanza wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya mifugo na uvuvi na kusema, masoko yote yaweke wazi tozo zote ambazo mfanyabiashara anatakiwa kulipa pindi anunuapo bidhaa.

Amesema kuwa viongozi husika lazima wajue na kutambua majukumu yao bila kusubiri Waziri kuja kukagua maendeleo ya masoko na hivyo kuwataka maafisa na wafanyabiashara kukaa na kupanga mikakati ya kuongeza mapato ya Serikali.

Aidha, kuhusu udhibiti wa uvuvi haramu Ulega amewapongeza wavuvi kwa kutii sheria bila shuruti kwani hakuna nyavu haramu iliyokamatwa katika ukanda wa ziwa Victoria na Kayenze.

Hata hivyo, Ulega amewashauri wafanyabiashara kujua tozo wanazotakiwa kutoa kabla ya kununua mizigo kwani itawasaidia sana katika ufanyaji wao wa biashara kwa kutambua kiasi wanachotakiwa kulipa kama tozo kuliko kutoa tozo bila kujua nj kiasi gani wanatakiwa kulipa.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 27, 2018
Vyama vya Upinzani vyasusia uchaguzi Tanga