Kiongozi wa chama kikuu cha Upinzani nchini Kenya cha ODM, Raila Odinga hivi karibuni alikumbwa na bahati mbaya baada ya jukwaa alilokuwa akilitumia kuhutubia kuporomoka na kuwamwaga chini yeye na viongozi wengine wa chama hicho.

Tukio hilo la kusikitisha kwa Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Kenya, lilitokea katika viwanja vya Karisa Maitha mjini Malindi, jimbo la Kilifi katika pwani ya Kenya siku moja kabla ya Siku Kuu ya Ijumaa Kuu, inayokumbukwa na Wakristo wote duniani kama siku ya kumbukumbu ya kuteswa na kufa kwa Yesu Kristo.

Akitoa simulizi la namna Yesu alivyoshinda vishawishi vya Shetani alipokuwa duniani, Raila Odinga alijikuta akishindwa kumalizia simulizi lake kutoka kwenye Biblia baada ya Jukwaa kuporomoka.

Video ya tukio hilo imekuwa gumzo kwenye mitandao Afrika Mashariki kwa kipindi cha hivi karibuni.

Magufuli apitisha Panga lingine huku
Waliompiga Daktari Washushiwa Rungu