Mshambuliaji wa Tanzania, Thomas Ulimwengu amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea klabu ya JS Saoura ya Algeria.

Amesaini mkataba huo ambapo klabu yake hiyo ipo miongoni mwa timu 16 zilizoingia hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika sambamba na Simba SC ya Tanzania.

Usajili huo wa Ulimwengu umekuja ikiwa ni miezi miwili tu imepita tangu avunje mkataba na klabu ya Al Hilal ya Sudan ambayo hata hivyo hakuweka wazi sababu za kuvunja mkataba na timu hiyo ndani ya miezi mitatu tu.

Aidha, klabu ya JS Saoura imethibitisha usajili huo kwa kuweka picha ya Ulimwengu akiwa na mabosi wa timu hiyo akikabidhiwa jezi tayari kwa kukipiga.

Ulimwengu huenda akakutana na Simba kwenye hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika kama ilivyokuwa kwa Yanga kwenye hatua ya makundi ya kombe la shirikisho mwaka 2016 alipokuwa akichezea TP Mazembe.

Maaskofu wapigilia msumari vita ya ushoga, CCM yawaangukia marafiki wa Lowassa
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 26, 2018