Mwandishi na mchambuzi nguli wa masuala ya kisiasa nchini, Jenerali Ulimwengu amekosoa mwenendo wa demokrasia nchini akieleza kuwa ingawa Serikali imefanya kazi kubwa ya kurejesha matumaini ya wananchi, katika suala la demokrasia tumerudi nyuma kwa miaka 50.

Jenerali Ulimwengu ametoa kauli hiyo leo wakati akichangia katika Kongamano la Kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es  Salaam.

Jenerali Ulimwengu ambaye pia ni Mwanajopo la Wataalam la Baraza la Habari Tanzania (MCT) alisema kuwa kumekuwa na ukandamizaji mkubwa wa vyombo vya habari, haki ya kujieleza na kukusanyika pamoja na kuficha uhuru wa wakilishi wa Wananchi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Pamoja na hatua zote nzuri anazochukua rais wa Sasa hivi, Dk. John Pombe Magufuli ambazo zimepongezwa, lakini ukiangalia ile picha kubwa ya nchi hii ni kwamba tumerudi nyuma miaka 50 katika masuala ya kidemokrasia,” alisema Jenerali Ulimwengu.


Naye Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliwataka viongozi wa Serikali kuiga mfano wa Mwalimu Julius Nyerere kuwaomba radhi wananchi pale wanapokosea, huku akitoa mfano wa Mwalimu kuwaomba watanzania wote radhi wakati alipokuwa anang’atuka urais.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali, wanazuoni, wanaharakati na wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii huku msemaji mkuu akiwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa.

Lowassa amuamkia IGP Mangu
Meya wa Jiji la Mwanza akimbia Ofisi baada ya ‘AC’ kutoa hewa yenye ‘Sumu’