Jeshi la polisi Tanzamia limesema sikuku ya Eid el Fitri itasherehekewa huku dunia ikiwa imekumbwa na janga la ugonjwa wa Covid 19, hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Msemji wa jeshi la polisi, David Misime imeeleza kuwa Jeshi la Polisi limetoa wito na msisitizo mkubwa kwa Watanzania kusheherekea huku wakizingatia kimamilifu maelekezo yaliyotolewa na wataalamu wa afya ya namna ya kujikinga na Corona.

Bendera ya Marekani yashushwa nusu mlingoti, maombolezo vifo vya corona

“Tuna uhakika kila mmoja kuzingatia maelekezo hayo kuanzia ngazi ya familia, mafanikio makubwa ambayo tumeanza kuyapata katika kukabiliana na ugonjwa huu nchini kwetu ,” imesma taarifa hiyo

Hata hivyo Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inakuwa ni ya uhakika na kwamba waumini wa dini ya Kiislamu na Watanzania wote wanasherehekea katika mazingira ya amani na utulivu.

Wahudumu wa afya 10,000 waambukizwa corona Iran

Burundi watakiwa kuwa watulivu, matokeo wiki ijayo

Wabunge wawili wa CHADEMA watimkia NCCR- Mageuzi
Miraji awatumia ujumbe huu mashabiki