Kama wewe ni mmoja kati ya watu ambao walibaki midomo wazi baada ya mtoto wa Diamond na Zari, Tiffah kupata michongo ya mamilioni ndani ya siku chache tu alipozaliwa pamoja na wafuasi lukuki kwenye Instagram, ni dhahiri ya mapacha wa Jay Z yatakustaajabisha.

Familia ya Bwana Shawn ‘Jay Z’ Carter imeripotiwa kuajiri wahudumu 18 nyumbani kwao kwa ajili ya kuwahudumia watoto wao mapacha, Sir na Rumi waliozaliwa mwezi Juni mwaka huu.

Chanzo cha kuaminika kimeuambia mtandao wa Radar Online kuwa kati ya waajiriwa hao wapo ‘mayaya’ sita, wahudumu wa ndani wawili na timu ya ‘manesi’ wanaobadilishana 24/7.

Mapacha hao ambao hawajajua nini kinaendelea duniani, wamepewa wataalam wa mitandao ya kijamii watakaoshauri kuhusu utumiaji wa mitandao ya kijamii. Wataalam hao watakuwa na kazi ya kuanzisha majina na tags zitakazotumika kwenye mitandao ya kijamii kuwakilisha mabosi wao, Sir na Rumi.

“Rumi na Sir hadi wana washauri wa masuala ya kifedha na uwekezaji wanaofanya kazi kwa ajili yao tu. Hao kazi yao ni kushughulikia jinsi majina ya watoto hao yanavyoweza kuingiza fedha na kutengeneza nembo za biashara,” Radar Online wameelezwa.

“Timu ya ulinzi ya mapacha hao imeajiriwa na kukabidhiwa gari maalum lenye uwezo wa kuzuia risasi kupenya (bullet proof),” chanzo hicho cha karibu na familia ya Jay Z kimekaririwa.

Kama ilivyokuwa kwa Tiffah wa Diamond ambaye alikaribishwa Madale kwenye jumba la wazazi wake lenye gharama kubwa likiwa na nakshi za dhahabu hadi jikoni, Jay Z na Beyonce wamewakaribisha mapacha wao katika jumba lao jipya la kifahari lililoko Malibu lenye thamani ya dola za kimarekani milioni 25 (zaidi ya bilioni 55 za kitanzania).

Beyonce aliweka picha ya mapacha wake kwa mara ya kwanza kwenye instagram, Julai 14 mwaka huu na kuandika ujumbe kuwa mapacha hao wana umri wa mwezi mmoja.

Video: Polisi wamvuruga Lissu, Magufuli azuia Warundi kupewa uraia nchini
Kichanga akutwa hai baada ya kutelekezwa akiwa ndani ya box la viatu