Hesabu inawapa homa kali watu wengi sio tu Tanzania bali duniani kote, lakini wanaoikomalia na kuiweza huwa na nafasi kubwa ya kusherehekea mavuno hususan katika karne hii ya Sayansi na Taknolojia isiyowezekana bila hesabu.

Pie ni 22/7 au 3.14, formula ambayo huunganishwa katika njia ya kupata eneo la miduara mbalimbali kimahesabau.

Maajabu ya ‘Pie’ ni kwamba ni tarakimu zinazopatikana baada ya kugawanya 22/7 zinaweza kufikia mabilioni kadhaa lakini haziishi. Lakini pia, ingawa 3.14 ni namba iliyokadiriwa kuwakilisha 22/7, ukijaribu kuirudisha kwenda kwenye sehemu haitakupa 22/7 japo ukizitumia namba hizo kwa desimali au sehemu utapata jibu lako bila shaka.

Leo, Machi 14 ni siku ambayo dunia nzima huadhimisha siku ya Pie, siku ambayo iliasisiwa kwa mara ya kwanza mwaka 1988 na Larry Shaw, mwana mahesabu aliyekuwa akiishi San Francisco, Marekani.

Mwaka 12 mwaka 2009, Serikali ya Marekani iliitambua rasmi Machi 14 kama siku maalum ya ‘Pie’. mwaka 2010 Google iliitangaza siku hiyo na kuweka alama maalum za ‘Pie’ kwenye mitandao yake.

 

Esther Bulaya azidi kumtesa Wassira
Apple yaandaa simu isiyoweza kudukuliwa, kupekuliwa na Serikali yoyote