Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu amesema utaratibu wa upimaji wa kifua kikuu na Ukimwi bar kwa bar sio wa lazima, ila watatumia ushawishi kuhakikisha wananchi wanapima na kujua afya zao.

Ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 30 ya Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi (NACP).

”Tutatekeleza mpango wetu wa kupima TB na Ukimwi kwenye bar ila hautakuwa wa lazima, tutakachofanya ni kuwashawishi wananchi kutumia fursa ya kusogezewa huduma hiyo” amesema Ummy.

Aidha ameongezea kuwa Wizara ipo katika mkakati wa kubadilisha sera na sheria za Ukimwi na kuruhusu mtu aweze kujipimwa mwenyewe na kutoa fursa kwa vijana kuanzia miaka 15 kujipima wenyewe bila ridhaa ya wazazi.

Hatua hizo ni kufuatia serikali kutaka kubainisha na kuwatambua watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi pamoja na TB

 

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Mei 14, 2018
Mama ni Mungu wa duniani, heri ya siku ya kina mama duniani

Comments

comments