Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu ameielekeza Tume ya Utumishi wa waalimu nchini kuhakikisha wanafanya msawazo wa waalinu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuweka uwiano sawa wa waalimu nchini.

Akiongea na Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa waalimu Jijini Dodoma Waziri Ummy amaesema kumekuwepo na changamoto kubwa kwa baadhi ya shule kuwa na waalimu wengi huku nyingine zikikosa waalimu, hivyo ni wajibu wa tume kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa kwa wakati.

Waziri Ummy, amesema kuna baadhi ya shule zina watoto wengi lakini waalimu ni wachache huku shule nyingine zikiwa na waalimu wengi wanafunzi wachache, ni vyema kukawa na uwiano ulio sawa katika shule zote nchini.

‚ÄúTunafahamu kuwa zipo shule ambazo zinawaalimu wachache hasa maeneo ya vijijini, lakini nyingine zinawaalimu wengi, suala hili halikubaliki, suala hili linahitajika kufanyiwa kazi ingawa mara nyingi serikali inaangalia idadi ya wanafunzi,” Amesema Waziri Ummy.


Hata hivyo Amesema kutokufanya msawazo nikutokutenda haki kwa wanafunzi walioko vijijini hasa katika maeneo ya pembezoni ni wajibu wa tume kuhakikisha shule zote zinakuwa na idadi sawa ya waalimu

Aidha amewaelekeza Tume ya Utumishi wa Waalimu nchini kutumia mifumo ya kielektroniki katika kutatua kero za waalimu nchini ili kupunguza changamoto hizo kwa haraka na kutoa mrejesho kwa waalimu kwa wakati

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 9, 2021
Majaliwa atoa maagizo kwa Mawaziri na Makatibu wakuu