Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Ummy Mwalimu leo Jumatano Novemba 24, 202 ametangaza wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022 huku ikisema imawapa kipaombele wanafunzi wa vijijini shule za kitaifa za bweni.

Katika upangaji wa mwaka huu wanafunzi wote 907,802 waliofaulu mtihani wamepangiwa kuanza masomo Januari 17, 2022 kwa wakati mmoja baada ya maandalizi ya Serikali.

“Wanafunzi waliopangiwa shule za bweni za Kitaifa ni 1989 na hapa tumechukua zaidi wanafunzi wa vijijini lakini kwenye majiji na halmashauri tumeangalia sana wenye uhitaji tu,” amesema Mwalimu.

Waziri ametoa sababu za kupangiwa zaidi kwa wanafunzi wa vijijini katika shule za bweni za Kitaifa kwamba kunatokana na uamuzi wa Serikali wa kujali wanafunzi wote wapate elimu.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy, mpango wa kupanga nafasi hizo unakwenda kusaidia wanafunzi ambao huwa kwenye mazingira magumu na vikwazo ili wasome.

Wakati huo Waziri ametoa agizo kwa wakuu wa shule kote nchi kuacha visingizio vya michango au sare kwa wanafunzi wanaoanza bali waachwe waendelee na masomo huku mambo mengine watakamilisha mbeleni.

Mike Tyson aombwa kuwa balozi wa Bangi Malawi
Ndalichako: Waliokatisha masomo kwa ujauzito kurudi shuleni