Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu ametoa ripoti ya Uchunguzi wa Maabara ambapo amesema mashine moja ya kupima Covid 19 imekutwa na hitilafu na viongozi hawakuifanyia matengenezo kwa wakati.

Amesema kuwa mapungufu yamegunduliwa katika mfumo wa kimuundo, kiutendaji na uendeshaji wa kitaaluma katika upimaji wa vipimo, uhakiki wa ubora wa majibu na udhaifu kwenye kuhifadhi vipimo.

Aidha,Waziri Ummy amesema upimaji wa virusi vya corona umehamishiwa katika maabara mpya iliyopo Mabibo Dar es salaam ambayo itafahamika kama Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii.

Amesema kuwa Maabara hiyo mpya ina uwezo wa kupima sampuli 1,800 kwa saa 24 tofauti na ya awali iliyokuwa inapima sampuli 300.

Frankfurt: Waumini 40 waambukizwa Corona baada ya ibada
Uhuru Kenyatta atangaza mpango wa kuchochea uchumi