Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amelaani vikali vitendo vya ukatili vinavyofanywa dhidi ya watoto katika jamii na kusema hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kufanya hivyo.

Ummy amesema kama jamii inawajibu wa kuhakikisha watoto wanaishi, kukua na kuendelezwa katika mazingira salama na rafiki kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009.

Hivyo amewaomba wazazi, walezi na walimu kutambua wajibu wao mkubwa uliopo wa kuwafundsha na kuwalea watoto kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa kwani vitendo vya ukatili dhidi ya watoto havikubaliki katika jamii na ni kinyume cha sheria.

Ummy amezungumza hayo kufuatia sakata la mwanafunzi wa darasa la tano kucharazwa bakora mpaka kufa jambo lililozua tafran mkoani Bukoba na watanzania kwa ujumla kutokana na unyanyasaji huo mkubwa uliofanywa na mwalimu wa shule ya msingi huko mkoani Bukoba.

Aidha kumekuwa na mfulululizo wa matukio ya ukatili kwa watoto yakiwemo yale ya unyanyasaji wa kijinsia kama lile lilotokea shule ya sekondari St Florence jijini Dar es salaam.

Southgate atangaza jeshi litakaloivaa Hispania, Uswiz
Video: JPM afunguka kuhusu sakata la Makontena ya Makonda