Hospitali ya Rufaa ya Taifa  ya Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa magari mawili ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya shilingi  milioni 80 kutoka ubalozi Wa Japan kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Akipokea msaada  wa magari hayo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa anashukuru kwa msaada huo kwani utarahisisha huduma kwa wagonjwa wa hospitali hiyo.

“Nashukuru  kwa msaada uliotolewa na serikali ya Japan na wasichoke kutusaidia katika kuboresha sekta ya Afya nchini” alisema  Mhe. Ummy.

Kwa upande wa Balozi Wa Japan Bw. Masaharu Yoshida amesema kuwa hawatachoka kutoa msaada kwa Tanzania ili kuboresha sekta ya afya na kuweka mahusiano bora kati ya Japan na Tanzania.

” Hatutachoka kutoa msaada kwa Tanzania kwani tunaboresha sekta ya afya na kudumisha mahusiano yetu” alisema Bw. Yoshida

Kwa wakati huohuo Waziri Ummy amepokea gari lingine la kuwabebea watoto kutoka kwa kampuni ya Bango Sangho ili kurahisisha  kuwapeleka katika kliniki mbalimbali jijini Dar es salaam.

Akikabidhi gari hilo Mwenyekiti wa kampuni ya Bango Sangho Bw. Niladri Chowdhury amesema kuwa wameamua kutoa msaada huo ili kuwarahisishia watoto kupelekwa kliniki kwa haraka pindi inapohitajika na kuokoa maisha yao.

Mbali na hayo Waziri Ummy pia amezindua bodi ya udhamini katika hospitali ya Muhimbili amabayo itadumu kwa muda wa miaka mitatu ili kufanya huduma za ya hospitali hiyo kuwa bora zaidi kwa maendeleo ya sekta ya afya nchini.

Akizungumza katika uzinduzi Wa bodi hiyo Mhe. Ummy  amesema kuwa bodi hiyo iwe ya  kiutendaji na kutatua matatizo ya wagonjwa na sio kua kero kwa wafanyakazi na wananchi.

Aidha Waziri Ummy ameitaka bodi hiyo kufanya kazi kwa kushirikiana na wizara pamoja na menejimenti ya hospitali hiyo ili kuleta huduma bora za kiafya kwa maendeleo ya taifa letu kwa ujumla.

Kwa upande wa Mwenyekiti mpya wa bodi ya udhamini ya MNH Dkt. Charles Majinge amesema kuwa amepokea nafasi hiyo kwa mikono miwili na kuahidi kuleta mabadiliko katika sekta ya afya nchini kwa kushirikiana na Wizara.

“Licha ya changamoto zilizopo nimeipokea nafasi hii kwa mikono miwili na kuhaidi kuleta mabadiliko katika sekta ya afya nchini kwa mda uliopangiwa ili kuleta maendeleo ya huduma bora kwa jamii.

Raisi Magufuli Apokea Hati Za Utambulisho Wa Mabalozi Kutoka Nchi Mbali Mbali
Ummy Mwalimu Azindua Ujenzi wa Jengo La Hospitali Ya Aghakan