Serikali imeuomba uongozi Wa Agakhan kujenga hospitali nyingine kubwa katika mkoa Wa Dodoma ili kuendana na agizo la Rais Wa awamu ya tano Dkt.John Magufuli na kuboresha huduma bora za afya Mkoani humo.

Akizungumza hayo wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya jengo la hospitali ya Agakhan Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu amesema kuwa Agakhan wanatakiwa wajenge hospitali nyingine kubwa mkoani Dodoma ili kueneza Huduma bora za kiafya.

“Kutokana na Agizo la Rais Wa awamu ya tano Dkt. John Magufuli la kuhamia Dodoma inabidi na nyinyi mjenge hospitali kule” alisema Mhe. Ummy.

Mhe. Ummy ameongeza kuwa kwa kujengwa hospitali hiyo Serikali itakua iokoa shilingi billion 20 mpaka 25 kwa ajili ya wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Aidha Mhe.Ummy amesema kuwa anaushukuru uongozi Wa Agakhan kwa kuanza kujenga jengo ilo linalogharimu Billioni 112 ili kuondoa kero kwa wagonjwa Wa magonjwa yasioambukiza na kurahisiaha huduma na matibabu bora kwa wagonjwa nchini.

Mbali na hayo Mwenyekiti wa kamati ya bodi hospitali ya Agakhan Bi. Zahra Aga Khan amesema kuwa wanampango Wa kumaliza jengo hilo kwa ajili ya kutoa Huduma bora za kiafya  nchini ili kutokomeza maradhi ya mara kwa mara.

“Tuna morali kubwa ya kumalizia jengo hili ili tuweze  kuboresha Huduma ya afya nchini kwa kutoa tiba zenye uhakika na za kisasa” alisema Bi Zahra

Ummy Mwalimu Apokea Gari La Kubebea Watoto Muhimbili
Claudio Ranieri Apandwa Jeuri, Ni Baada Ya Kuyabakisha Majembe Yake