Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia  Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ametoa rai kwa viongozi wa Dini nchini kuhakikisha wanaepuka misongamano kwenye nyumba za ibada hasa katika kipindi hiki cha kuelekea sikuku ya Pasaka ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo April 9, 2020 wakati wa kikao cha kitaifa cha viongozi wa Dini kilichozungumzia jinsi ya kujikinga namaambukizi ya virusi vya Corona.

Waziri Ummy amewaomba viongozi wa dini zote kuhakikisha kuwa  waumini wenye dalili za kikohozi, mafua na homa, wanabaki nyumbani.

” Ni mategemeo yetu viongozi wadini kuepuka mikusanyiko ya watu wengi tunategemea kupata ushirikiano wenu kuhakikisha kuwa ibada inaendeshwa katika hali ambayo si hatarishi, Rais ameeleza kuwa serikali haitafunga nyumba za ibada lakini wajibu wetu kuangalia sasa tutafanyaje ibada kwa namna ambayo si hatarishi kwetu na kwa waumini” amesema ummy

Aidha amewataka viongozi hao wa dini kutumia teknolojia katika mikutano yao ili kukwepa mikusanyiko.

 

 

Carlos Alberto Tevez Apache - Nabii anayekubalika kwao
Haji Manara ashindilia msumari Bilioni 20 Simba SC