Vyombo vya Habari Nchini Vimetakiwa kujiepusha na taarifa ambazo zinaweza kuichonganisha Serikali na wananchi kwani kufanya hivyo kunaweza kuleta machafuko au chuki baina ya Serikali na wananchi wake.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa kituo cha Redio cha Voice of Africa kilichopo Korogwe Mkoani Tanga.

Ummy amesema kuwa wanahabari wanapaswa kuzingatia maadili ya kazi yao, pia kutengeneza vipindi vya kutoa elimu pamoja na habari zenye uhakika, vitu ambavyo huleta heshima  ya taaluma.

“Serikali hatukatai kukosolewa ila mtoe taarifa zenye ukweli ili sisi kama wahusika, tuzifanyie kazi ila siyo kutuchonganisha na wananchi”amesema Ummy.

Waziri Ummy amesema kuwa Serikali haikatai kukosolewa na vyombo vya habari,ila habari zinazoandikwa zinatakiwa zizingatie weledi, ziwe za uhakika na zenye ukweli.

Mwana FA, Darassa ‘watoana nduki’ YouTube
Sheikh Ponda ateta na Lema kwa dakika 60 gerezani, ampongeza kukaa mahabusu