Viongozi wa Dini nchini Kenya, wametakiwa kusimama imara kurejesha umoja wa kitaifa kufuatia wimbi la mpishano wa Viongozi wa Kenya kwenye nyumba za ibada kushukuru kwa kuchaguliwa na wa upinzani wakiendelea kulalamika kuhusu kuibiwa kura wakati wa uchaguzi.

Akiongoza mkutano wa maombi ya shukrani uliowakutanisha pamoja Viongozi wa kisiasa, mawaziri, viongozi wa kidini na maafisa wakuu wanaohudumu katika kaunti ya Nakuru, Gavana Susan Kihika aliwahimiza viongozi wa kidini kudhihirisha mchango wao kwa umma na kuwapa mwongozo.

Mchango wa kanisa kwenye siasa za Kenya, umezusha mdahalo hasa baada ya kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja one Kenya, Raila Odinga kumkosoa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kianglikana, Jackson Ole Sapit, kwa kuhusika kwenye siasa na kuegemea upande wa Rais William Ruto, wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti 2022.

Hata hivyo, Askofu huyo Mkuu huyo wa Kanisa la Anglikana nchini Kenya, ametoa wito kwa wanasiasa kupunguza malalamiko na badala yake kuzingatia muunganiko wa Wakenya na namna ya kuboresha hali ya uchumi wa Wakenya huku akihimiza usawa baina ya viongozi walioko serikalini na wale wa upinzani.

Sekta ya Uvuvi yatengewa Bil. 60 kuhamasisha ufugaji wa samaki
Wataalamu Mawasiliano watakiwa kulitumikia Taifa kwa weledi