Viongozi wa Afrika wameulaani mpango wa amani ya Mashariki ya Kati uliopendekezwa na Rais wa Marekani, Donald Trump kwa kusema si halali.

Akizungumza na viongozi wakuu wa mataifa ya Afrika kwenye mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja huo, Moussa Faki Mahamat, amesema mpango huo uliotangazwa mwishoni mwa mwezi uliopita unawakilisha uvunjaji usio kipimo wa maazimio mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Mahamat amesema mpango wa Trump uliandaliwa bila kushauriana na Jumuiya ya Kimataifa na kwamba unazikandamiza haki za Wapalestina.

Mpango huo uliopewa jina la Makubaliano ya Karne, ulikataliwa tangu mwanzoni na Wapalestina wakiungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa na mataifa jirani ya Mashariki ya Kati, Ghuba na Ulimwengu wa Kiislamu.

Wanajeshi wavamia Bunge kushinikiza muswada kupitishwa

Mwenyekiti Faki ametaka viongozi waelekeze macho yao kwenye chanzo cha migogoro iliyopo Afrika na “kutafuta masuluhisho yenye kuliweka suluhisho la kijeshi kwenye mwelekeo wake kwa kulichanganisha na hatua za maeneo mengine, hasa hasa maendeleo.”

Viongozi wa mataifa ya Afrika wamekutana kwaajili mkutano wa kilele katika makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa, kujadili dhima ya chombo hicho kwenye utatuzi wa migororo ndani ya bara hilo na umebeba maudhui “Kunyamazisha Bunduki”, lengo lililoamuliwa mwaka 2013 la “kukomesha vita vyote barani Afrika ifikapo mwaka 2020”.

Samia: Migogoro AU inachelewesha maendeleo
Wanajeshi wavamia Bunge kushinikiza muswada kupitishwa