Wakati ambapo harakati za kampeni za uchaguzi mkuu zikizidi kupamba moto zikiwa zimebaki takribani wiki mbili na nusu, Umoja wa Mataifa umetoa mtazamo wake kuhusu picha ya uchaguzi mkuu na wagombea wanaowani nafasi ya urais.

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Balozi Alavaro Rodriguez amesema kuwa picha ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni ngumu kuitabiri kutokana na mabadiliko makubwa yanayoonekana.

Balozi Alavaro alisema kuwa hata tafiti mbalimbali zilizofanyika hivi karibuni nchini, matokeo yake hayakutosha kutoa picha halisi ya uchaguzi hususan nafasi ya urais na nani ataibuka kuwa mshindi.

Aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wahariri wa gazeti la Mwananchi katika ofisi za watayarishaji wa gazeti hilo, ambapo aliambatana na Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu.

“Yametokea mabadiliko katika siasa za ndani. Kinachoendelea hivi sasa kisingeweza kutabiriwa miezi mitano iliyopita. Kinachoonekana ni kama siasa za Tanzania zinategemea sana ushawishi wa mtu mmoja mmoja,” alisema Balozi Alvaro.

“Zaidi ya watu milioni 23.7 walijiandikisha kati ya 24 milioni walikadiliwa na NEC, inadhihirishwa kulikuwa na maandalizi ya kutosha na elimu ya kutosha ilifika kwa wananchi. Lakini tafiti zilizotangazwa mpaka sasa sio za kutosha kuweza kutoa picha ya nani anaweza kuibuka mshindi baada ya kura kupigwa,” aliongeza.

 

Lowassa Ageukia Mikopo Ya Vyuo Vikuu, Atangaza Neema Kwa Wote
Marbury Amchana Hadharani Michael Jordan