Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kutetea haki za binadamu, Michelle Bachelet ameilaani vikali hatua ya Saudi Arabia ya kutekeleza hukumu za kifo.

Saudia ilitekeleza hukumu hiyo ya kifo kwa kuwakata vichwa watu 37 katika miji sita nchini humo.

Wizara ya Mambo ya ndani ya Saudia ilisema watu hao ambao wote ni raia wa Saudi Arabia walinyongwa kwa kuhusishwa na masuala ya ugaidi.

Aidha, Bachelet amesema kuwa amesikitishwa na kutofuatwa kwa sheria na utaratibu wa kimahakama kutokana na madai kuwa watuhumiwa hao walikiri kujihusisha na ugaidi baada ya kuteswa.

Hata hivyo, ameutaka uongozi wa Saudi Arabia kuangalia upya sheria za kupambana na ugaidi na kusimamisha mauaji yaliyokuwa yamepangiwa kufanywa, yakiwemo ya watu watatu ambao bado wanakabiliwa na hukumu ya kifo.

Kimbunga Keneth tayari kimetua Msumbiji
Viongozi wakuu wa Baraza la Mpito la Kijeshi wajiuzulu Sudan