Ripoti iliyotolewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imebainisha kuwa Korea Kaskazini haijasitisha mpango wake wa kinyuklia pamoja na ule wa kutenegeneza silaha, kitendo kinachokiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa .

Ripoti hiyo imesema kuwa Pyongyang imeongeza idadi ya meli zinazosafirisha bidhaa za mafuta na imekuwa ikijaribu kuuza silaha nchi za nje.

Aidha, ripoti hiyo ya siri iliyoandaliwa na jopo la wataalamu mbalimbali iliwasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa.

Hata hivyo, Korea Kaskazini hadi kufikia sasa haijatoa tamko lolote kuhusu ripoti hiyo.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 5, 2018
Skimu za umwagiliaji kuinua uchumi wa viwanda nchini