Umoja wa mawakala wa pembejeo za kilimo nchini wamemuomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli kukutana nao ili kuweza kulipatia suluhu suala linalowakabili la madai ya fedha wanazoidai Serikali kwa ajili ya usambazaji wa pembejeo katika msimu wa mwaka 2015/2016.

Hayo yamesemwa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Umoja wa Mawakala wa pembejeo za kilimo nchini, Gerald Mlenge wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu malalamiko ya madai yao kwa Serikali.

Amesema wanaomba kukutana na Rais Dkt. Magufuli ili waweze kumweleza ukweli na aweze kulitafutia ufumbuzi jambo lao hilo ambalo limekuwa likiwasumbua kwa muda mrefu.

“Rais Magufuli tafadhali kama unatusikia tunakwambia juu ya zoezi hili na jinsi linavyoendeshwa ukweli tunao sisi mawakala, tunaoitwa wezi badala ya kutuambia kuwa wadanganyifu sasa wewe utuite tukwambie na mengine Rais tunakuomba, tunaomba viongozi wote wa Wizara ya Kilimo hasa wale wasimamizi wa kitengo cha pembejeo za ruzuku katika kikao chako nao wawepo ili tuongee yote ya moyoni ili wewe uweze kutoa maamuzi yako kwa haki juu ya malipo yetu sisi tunaoteseka,”amesema Mlenge

Hata hivyo Makamu Mwenyekiti wa umoja huo, Idd Madeni amesisitiza kuwa wao wana mambo mengi ya kusema lakini hawana sehemu ya kuyasema mambo ambayo wanakutana nayo.

Mtatiro: Bora CCM kuliko kufanyakazi na Prof. Lipumba
Mkasa: Waliniambia nina roho ya Paka mbona sifi, nilipigwa kuanzia saa 4 - 12 (Video)