Umoja wa Ulaya umeikosoa Uganda kwa namna maafisa wa usalama walivyo wakamata wabunge na raia kaskazini mwa nchi hiyo kwa madai kuwa waliushambulia kwa mawe msafara wa Rais Yoweri Museveni.

Taarifa ya wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya waliopo jijini Kampala inataka kuchukuliwa hatua wote walioshiriki katika kuwapiga wabunge na raia katika mazingira yanayotajwa kuwa ni ya kinyama.

Msemaji wa serikali wa nchi hiyo, Ofwono Opondo amekanusha taarifa kwamba wabunge na raia walipigwa, akieleza kuwa maumivu wanayopata wahusika, huenda yanatokana na nguvu zilizotumika wakati walipokuwa wakikamatwa.

Aidha, taarifa ya Umoja wa Ulaya imekuja wakati Wakili wa Mbunge, Robert Kyagulanyi maarufu ‘Bobi wine’ akiripoti kuwa mbunge huyo, anayeshikiliwa katika gereza la kijeshi la Makindye jijini Kampala, hawezi kuongea, kusimama wala kukaa baada ya kupigwa vibaya na kikosi kinachotoa ulinzi kwa Rais Museveni SFC.

Hata hivyo, Bobi Wine, na wabunge wengine sita, wamefunguliwa mashtaka ya kutaka kupindua serikali ya Rais Museveni kufuatia vurugu zilizozuka, siku ya mwisho ya kampeni katika uchaguzi mdogo wilayani Arua, kaskazini mwa Uganda.

Video: Kivumbi cha sh tril. 1.5 kutimka tena, Hamahama ya vyama yampa ukakasi Nape
Nape: Wanaohama vyama wananipa ukakasi mkubwa sana