Wakuu wa Nchi za Umoja wa Ulaya na Nchi 3 za Afrika wamekubaliana kuhusu mpango wa kupunguza idadi ya wahamiaji wanaoelekea Ulaya, na pia kukabiliana na uhamiaji haramu.

Mataifa manne yenye nguvu za ushawishi mkubwa barani Ulaya pamoja na nchi tatu za Afrika zimekubaliana kuwe na mpango wa kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu.

Aidha, kwa muda mrefu, Umoja wa Ulaya unaoundwa na nchi wanachama 28 umekuwa ukitafuta njia mbadala ya kuweza kukabiliana na wimbi kubwa la wahamiaji haramu ambalo limekuwa likimiminika barani humo.

Mwenyeji wa mkutano huo uliowakutanisha wakuu wa nchi za Ujerumani, Italia, Uhispania, Chad, Niger na Libya kujadili suala hilo, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kuwa wakati umewadia wa kuwa na mpangilio imara

Viongozi hao wamekubaliana kuwa na mpango wa pamoja wa kuanza kuwatambua wahamiaji halali wanaokimbia vita au waliopo katika kitisho cha kuuawa na kutumia Umoja wa Mataifa kuwasajili nchini Niger na Chad kama hatua ya kuwazuia dhidi ya unyanyasaji kutoka kwa wasafirishaji haramu wa binadamu.

 

Lissu aungwa mkono na Kituo cha Haki za Binadamu LHRC
Washikiliwa na Polisi kwa kosa la kufanya mapenzi na wanafunzi