Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema Umoja huo unaangalia njia bora ya kuzisaidia kujikwamua kiuchumi nchi za Afrika na zile zinazoendelea baada ya kuathirika na janga la UVIKO – 19 huku wakiendelea na jitihada za kuhakikisha chanjo za ugonjwa huo zinapatikana kwa usawa na kwa wote.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Balozi Liberata Mulamula ameyasema hayo baada ya kukutana kwa mazungumzo na Kiongozi huyo mwandamizi wa Umoja wa Mataifa katika Ofisi za Umoja huo zilizopo New York Marekani, mazungumzo yaliyolenga kuimarisha mahusiano,usawa wa jinsia pamoja na masuala mtambuka ya kipaumbele kwa maendeleo ya uchumi wa Tanzania

Balozi Mulamula ameongeza kuwa wamejadili kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utakaofanyika mwezi Septemba na ujumbe wa Tanzania utaongozwa na Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema Umoja huo kwa sasa unaendelea kutathmini hali ya maambukizi ya ugonjwa wa UVIKO -19 ili kufanya maamuzi ya endapo Mkutano huo ufanyike kwa njia ya mtandao ama vinginevyo.

Waathiriwa wa vita vya Yemen waitaka ICC kuchunguza madai ya uhalifu wa kivita
Wizara ya Habari,JWTZ kuboresha uhusiano wa kimichezo