Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepongeza uamuzi wa Rais Joseph Kabila kutowania muhula mwingine katika uchaguzi ujao wa DRC, na kusema uchaguzi huo unapaswa kupelekea makabidhiano ya amani ya madaraka.

Baraza hilo limevihimiza vyama hasimu vya siasa nchini humo, pamoja na taasisi zinazohusika na maandalizi ya uchaguzi huo wa mwezi Desemba mwaka huu, kuhakikisha kuwa zoezi la upigaji kura linakuwa la amani na la kuaminika.

Aidha, wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamewahimiza washiriki wote kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafanyika katika mazingira ya uwazi, uaminifu na ushirikishwaji.

Vile vile, wamesema kuwa kuheshimu haki za msingi na kusimamia kalenda ya uchaguzi ni mambo muhimu yatakayohakikisha uchaguzi wa amani hapo Desemba 23 mwaka huu.

Hata hivyo, Marekani, Ufaransa na Uingereza zilikuwa zimemuomba Rais Kabila kubainisha wazi kwamba hatowania muhula mwingine, wakati kukiwa na hofu kubwa kushindwa kwake kuachia madaraka kungeweza kusababisha vurugu.

Tabia mbaya usizozijua zinazozeesha katika umri mdogo
Mario Mandzukic astaafu soka

Comments

comments