Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ametoa wito kwa Syria kushtakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

Amesema kuwa mwezi Desemba hakuna misaada ya kiutu iliyofikishwa kwa zaidi ya watu 417,000 katika maeneo tisa yaliyozingirwa na waasi.

Aidha, ameongeza kuwa ni jambo la muhimu kwa Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wake kuwafikia watu wanaoishi katika maeneo yaliyozingirwa na waasi ili kuweza kuwapatia huduma za kibinadamu.

Vile vile ameligusia eneo la mashariki mwa Ghouta ambako bei za bidhaa za zimepanda mara 30 zaidi ikilinganishwa na mji wa Damascus, kitu ambacho kinawafanya raia wa eneo hilo kushindwa kujikimu.

Hata hivyo, Urusi na China zilipinga kwa kura ya turufu azimio la Baraza la Usalama lililoungwa mkono na nchi 60 mwezi Mei 2014 la kulifikisha suala la mgogoro wa Syria katika mahakama ya kimataifa.

Maamuzi kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi – Ligi kuu Tanzania bara
Rais Kabila atangaza tarehe ya uchaguzi