Umoja wa Mataifa umewapongeza viongozi wa Kenya baada ya kiongozi wa muungano wa Upinzani wa NASA, Raila Odinga kukutana na Rais, Uhuru Kenyatta kwa mara ya kwanza na kufikia makubaliano ya kuondoa mvutano wa kisiasa.

Hatua hiyo ya Raila Odinga imepokelewa kwa hisia tofauti na baadhi ya wanachama wa upinzani wanaohisi kitendo hicho ni usaliti.

Akizungumzia pongezi hizo kutoka Umoja wa Mataifa wakati wa mahojiano na DW, Mwanasheria na mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka nchini Kenya, Agina Ojwang amesema kuwa UN na taasisi mbalimbali wanaelewa kwa kina maana halisi ya mkutano kati ya rais Kenyatta na Odinga.

 

Video: Prof. Bana awataka Wanasiasa kuiga mfano wa Kenya
Aden Rage aihusia Simba kabla ya safari ya Misri

Comments

comments