Shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani (WHO), limezindua mpango unaolenga kukomesha kuenea zaidi kwa mbu wa malaria barani Afrika, huku ikionya kuwa zaidi ya asilimia 40 ya watu barani Afrika wanaoishi katika mazingira ya mijini, wanaweza athiriwa na mbu aina ya Anopheles stephensi, kwa kukosekana kwa udhibiti au kutokomeza ugonjwa wa malaria.

Kwa mujibu wa ripoti ya tahadhari ya mbu wa malaria iliyotolewa mwaka 2019, WHO ilibainisha kuenea kwa mmbu aina ya Anopheles stephensi kuwa ni tishio kubwa la juhudi za kudhibiti na kutokomeza malaria hasa katika Afrika, ambako ugonjwa huo ambao umewaathiri watu wengi zaidi.

Mbu hao, kwa asili hupatikana zaidi sehemu za Asia Kusini na rasi ya Arabia, lakini sasa Anopheles stephensi wamekuwa wakipanua wigo wake katika muongo uliopita, na kuliripotiwa kupatikana nchini Djibouti (2012), Ethiopia na Sudan (2016), Somalia (2019) na Nigeria (2020), na kwamba mbu hao hustawi katika mazingira ya mijini.

Dkt. Jan Kolaczinski, anayeongoza kitengo cha kudhibiti na kupambana na usugu wa viuatilifu katika mpango wa kimataifa wa Malaria wa WHO amesema “Bado tunajifunza kuhusu uwepo wa Anopheles stephensi katika maambukizi ya malaria barani Afrika, bado hatujui ni umbali gani aina ya mbu hawa tayari wameenea, na ni shida gani ambazo wameleta au wanaweza kusababisha.”

Pingamizi la Marekani kwa Urusi utwaaji maeneo Ukraine 'ladunda' UN
Msajili, Jaji, Wajumbe wala kiapo mbele ya Rais