Umoja wa mataifa umezindua mpango wa kuthibiti ugaidi kwa kufuatilia wasafiri ili kuimarisha ushirikianao wa kimataifa na kuongeza uwezo wa kubaini na kuzuia safari za magaidi

Uzinduzi huo umefanyika wakati wa kikao cha ngazi za juu kwenye makao makuu ya umoja wa mataifa New york Marekani kupitia ofisi ya kukabiliana na ugaidi  UNOCT.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema kuwa mpango huo unahusisha kuanzishwa kwa vitengo vya safari katika nchi husika, ambapo kwasasa kuna mienendo mingi inayohusisha wapiganaji wa kigeni na magaidi kusafiri kutoka kona moja hadi nyingine ya dunia.

Guterres ameongeza kuwa “Miaka miwili iliyopita tulikadiria kuwa na zaidi ya wapiganaji na magaidi wa kigeni 40,000, kutoka zaidi ya nchi 110 walisafiri kujiunga na makundi ya kigaidi nchini Syria na Iran”.

Amesema wengi wao wana mafunzo ya hali ya juu wanaweza kufanya mashambulizi na wengine wana matumaini ya kusaka wafuasi wapya, hivyo kuwabaini na kusambaratisha magaidi hawa na wahalifu wengine hatari kabla hawajafanya shambulio ni kipaumbele cha jamii ya kimataifa.

Kwa mujibu wa katibu mkuu mpango huo utasaidia nchi wanachama wa umoja wa mataifa kupunguza na kuzuia ugaidi kwa kubadilishana taarifa za mamlaka nyingine na kuheshimu faragha.

 

 

Masaa kadhaa ya R kelly kupigwa na kesi nyingine kubwa
Tahadhari, Mvua kunyesha kubwa zaidi mwisho wa wiki