Watu wengi husikika wakisema mapenzi matamu endapo wahusika wanapendana lakini pia ni shubiri pale ambapo hugeuka na kuwa tofauti na matarajio. Maisha ya mahusiano ni maisha ambayo kila kijana anaepevuka lazima atahitaji kuingia au kujaribu kujihusisha.

Hergo

Watu wengi wanao ingia kwenye mahusiano huwa hawapendi kukubali matokeo yanayotokea mara nyingi pale mambo yanapoenda ndivyo sivyo kwa kudhani kwamba  hawakustahili kufanyiwa hivyo  au kuona nafsi zao zinadhulumiwa,  Laa hasha!!! Ipo sababu ya  wewe kuendelea.

Wakati  mambo yanapokuzidia na usipojifunza kuacha yaende kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza utendaji kazi  wako unapokuwa ofisini  kwa kuwa tu maumivu ya mapenzi yatakuwa yanazunguka katika nafsi na ubongo wako.Pic1

 

Licha ya utendaji wa kazi kuwa hafifu lakini bado nafsi inahitaji kuwa na furaha na pindi furaha inapokosekana  kuna uwezekano mkubwa wa kupata maradhi tofauti tofauti wakati mwingine hata maradhi ya moyo, kwa sababu kuna jambo tu kubwa umelishika katika nafsi yako.

22

Kusema ndio kwenye furaha ni kujifunza kusema hapana kwa mambo na watu ambao wanakupatia mawazo. Huna budi kukubaliana na matokeo ya kumwacha aende zake ili uweze kuanza maisha mapya yenye furaha na amani huku ukiwa na tumaini mumgu atakuletea mwingine mwenye kujali hisia zako na kukupafaraja ya moyo.

 

.Go

Mbeya City Wasaka Vijana Wa Kujazia Kikosi - 2016-17
Madiwani wamtetea Kitwanga, Watoa tamko zito

Comments

comments