Mkwe wa kike wa rais wa Marekani Donald Trump, Vanessa Trump, alikimbizwa hospitalini kama tahadhari baada ya kufungua bahasha iliyokuwa na unga mweupe, Polisi wamesema.

Bahasha aliyofungua ilikuwa na barua iliyoelekezwa kwa mtoto kubwa wa kiume wa rais huyo, Donald Trump Jr, huko nyumbani kwake Manhattan.

Mke wa Trump mdogo na watu wengine wawili waliokuwepo kwenye eneo hilo la tukio walisafishwa kwanza na kikosi cha zimamoto na baadaye  kupelekwa hospitali kwaajili ya tathimini.

Polisi mjini New York (NYPD) wameieleza BBC kuwa wameupima unga huo mweupe uliokuwa kwenye bahasha na kuthibitisha haukuwa na madhara.

Wamesema kuwa, wamesema kuwa mke huyo wa  Trump mdogo hakuonekana kupatwa madhara yoyote ya kimwili kutokana na unga huo.

Katika ukurasa wake wa Twitter Trump Jr jana jioni aliandika kuwa familia yake iko salama na kuliita tukio hilo “ni baya”.

Kifaru amtambia Masau Bwire
Nyoka adaiwa kumeza mamilioni ya fedha

Comments

comments