Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Kenya limegawa redio 10,000 zinazotumia nishati ya sola kwa kaya masikini nchini humo ili watoto wengi wapate fursa ya kusoma nyumbani wakati huu wakijiandaa kurejea shuleni.

UNICEF limetoa msaada huo wa redio za sola baada ya kutambua athari za kufungwa shule wakati huu wa Covid-19 hasa kwa kaya masikini, ambapo watoto zaidi ya 40,000 watafaidika na mradi huo.

Mkuu wa Mawasiliano wa UNICEF nchini Kenya amesema kufungwa kwa shule kumeingilia masomo kwa mamilioni ya wanafunzi nchini humo ambao wamekosa masomo kwa zaidi ya miezi sita.

UNICEF imesema kwa wakati huo wote wameisaidia serikali na hata sasa katika maandalizi ya kufunguliwa shule kwa usalama.

Ingawa ni shule chache zimefunguliwa, UNICEF imesema inaendelea kusaidia wanaosomea nyumbani hadi pale shule zote zitakapofunguliwa.

Tetesi: Man City yaendelea kumuwinda Messi
Arteta: Sijabadili mipango ya usajili