Kundi baya la kigaidi linalojiita Islamic States of Iraq and Syria (ISIS), limeripotiwa kufanya unyama wa hali ya juu kwa kumkata kichwa msichana mwenye umri wa miaka minne mbele ya mama yake kwa kauli ya utani au kutokusudia aliyoitoa mama huyo.

Taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari kutoka Syria zimeeleza kuwa tukio hilo la kushtua na kusikitisha limetokea katika mji wa Raqqa nchini Syria unaodhibitiwa na kundi hilo lililoanzisha utawala wa sharia kali.

Imeelezwa kuwa Mama wa mtoto huyo aliapa kwa jina la ‘Allah’ bila kukusudia akimwambia mwanae huyo kuwa angemkata kichwa endapo angekataa kurudi nyumbani kutoka katika michezo na watoto wenzake mara moja, lakini ingawa  mtoto huyo alikataa kutekeleza amri hiyo kwa wakati hakutekeleza alichokuwa ameapa kufanya.

“Mama alimwambia binti yake wa miaka minne aende nyumbani na alikataa. Baadae, mama alimwambia ‘bila kukusudia’ kuwa ‘nenda nyumbani na naapa kwa Mungu kuwa nitakukata kichwa kama hutoenda’,” mwanamke mmoja aliyeweza kutoroka kwenye himaya ya ISIS alisimulia kisa hicho cha kusikitisha kupitia ‘Al Alam International News Channel’ ya Iran.

Alisema kuwa kiapo hicho ziliripotiwa kwa ISIS ambao wanatawala eneo hilo. Wanajeshi wa kundi hilo la kigaidi ambalo baada ya kumpata mama huyo walimtaka atekeleze kiapo chake kwa kumkata mwenyewe mwanae, ndipo walipotekeleza wao wenyewe.

“Lakini walimkata kichwa binti huyo mdogo na kumlazimisha mama yake kunawa damu za binti yake,” alisimulia mwanamke huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.

ISIS wamekuwa wakitekeleza mauaji ya kutisha katika nchi za Iraq na Syria kwa wakijaribu kupandikiza itikadi kali za sharia kwa kuwachinja wale wanaoenda kinyume nao.

Majeshi ya Marekani na washirika wake wameendelea kupambana na kundi hilo na kulidhoofisha kwa kiasi kikubwa katika miji wanayoishikilia.

Diamond awaweka mashabiki mguu sawa, kulipua Spika punde na ‘P Square’
Saba wafariki Dodoma kwa ugonjwa usiiojulikana