Kuna wakati binadamu wanafanya unyama hadi wanyama wenyewe wakipewa utashi kidogo watawaogopa na kuwashangaa.

Mwanamke mmoja nchini Brazil aliyetajwa kwa jina la Mirian Siqueria, anatafutwa na vyombo vya dola  akituhumiwa kumuua mjamzito mwenye umri wa miaka 15 na kunyofoa mtoto kwa lengo la kumuiba.

Kwa mujibu wa Mirror, msichana  aliyefanyiwa unyama huo aliyetajwa kwa jina la Valissia Fernandes de Jesus alikuwa na ujauzito wa miezi nane.

Polisi nchini humo wameeleza kuwa baada ya kumuua na kunyofoa kiumbe hicho kisicho na hatia, Mirian aliyekuwa anatafuta mtoto mchanga wa kumdanyia mumewe aligundua kuwa kichanga huyo alikuwa ameshapoteza maisha. Mwanamke huyo aliutupa chooni mwili wa mtoto huyo na kutokomea kusikojulikana.

Chanzo cha kutaka kuiba mtoto mchanga kwa njia hiyo ya kinyama kimeelezwa ni kutokana na kujifanya kuwa mjamzito muda wote akiwapa watu matumaini yasiyokuwepo kuwa atajifungua hivi karibuni.

Mirian Siqueira, aliyetafutwa

Mirian Siqueira, aliyetafutwa kwa mauaji

“Alikuwa akijifanya kuwa ana ujauzito wakati wote na baadae tulianza kugundua kuwa hakuwa na uwezo wa kupata ujauzito. Tumbo lake lilikuwa kubwa kwahiyo kila mtu alidhani kweli ni mjamzito. Alitayarisha chumba cha mtoto na alikuwa akiaga kuwa anaenda kuonana na daktari wake kila mwezi,” alisema Elida ambaye ni mtu wake wa karibu.

Mume wa Mirian alihojiwa na kituo cha runinga nchini humo na kueleza kuwa mkewe alipofika nyumbani alikiri kuwa alimchoma kisu Valissia lakini alisema alifanya hivyo baada ya kugombana.

“Mke wangu alikuwa akiniambia kuwa ana ujauzito. Lakini sasa hivi hata sijui alipo,” alisema mwanaume huyo.

Jeshi la polisi linaendelea kumsaka Mirian na kuchunguza tukio hilo lililotokea Jumatano wiki hii.

Fuvu la binadamu lakutwa ndani ya nyumba ya 'Mchungaji’
Mbunge wa Singida mjini Atoa Msaada wa Mashine ya kupima Malaria