Polisi wa Kaunti ya Kisumu nchini Kenya wanawatafuta wanaume 10 kwa tuhuma za kuwabaka wasichana wawili wanafunzi wa shule ya sekondari katika eneo la Ahero.

Wasichana hao walifanyiwa unyama huo majira ya usiku walipokuwa wanatembea kutoka kanisani wakielekea nyumbani. Walivamia na kubakwa karibu na eneo la kanisa.

Mratibu wa eneo la Nyando, Caren Omanga ambaye aliwapokea na kuwasaidia wasichana hao, alisema kuwa walitibiwa katika hospitali moja katika eneo la Ahero na hivi sasa wanaendelea na matibabu madogo-madogo wakiwa majumbani kwao.

Amewaambia waandishi wa habari kuwa walifanikiwa kumpata mwanaume mmoja aliyehusika, na kwamba Polisi wanamtumia kijana huyo kuwapata watuhumiwa wengine.

Omanga ameiambia Citizen TV kuwa ni lazima polisi wachukue hatua kuhakikisha wanakomesha ‘disco vumbi’ na matukio mengine ya starehe ya usiku yasiyo na vibali, ambavyo yameonekana kurejea baada ya kupigwa marufuku awali.

NEC yaamua rufaa zingine 49
Masau Bwire: ‘KUPAPASA NA KUKUNG’UTA’