Wakuu wa kikosi maalum cha jeshi la Guinea, wameahidi kuunda serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa baada ya kumuondoa madarakani Rais Alpha Conde Jumapili Septemba 5 .

Kikosi hicho kinachoongozwa na kanali Mamady Doumbouya kimemkamata Rais Conde na kuwapiga marufuku mawaziri na viongozi wengine wakuu kusafiri nje ya nchi.

Doumbouya hakutoa maelezo kuhusu watakaojumuishwa kwenye serikali hiyo ya mpito wala hakutangaza tarehe ya kuandaa uchaguzi ili kurejesha utawala wa kidemokrasia.

Wakati hayo yakijiri  jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika magharibi ECOWAS imesema itaandaa mkutano wa kilele siku ya Alhamisi kuhusu Guinea.

Mapinduzi hayo yamelaaniwa vikali na mataifa pamoja na mashirika ya kimataifa yakitia shinikizo kutaka Rais Conde aachiliwe huru.

Miundombinu ya TANESCO kutumika Mkongo wa Taifa
RC Makalla kusimamia maboresho mnada wa Pugu