Makamu mwenyekiti wa klabu ya Leicester City, Top Srivaddhanaprabha ameonyesha kufurahishwa na maamuzi yaliyotangazwa na Riyad Mahrez ya kuendelea kubaki King Power Stadium kama mkataba wake unavyoeleza.

Srivaddhanaprabha, amesema maamuzi yaliyoanikwa hadharani na kiungo huyo mshambuliaji kutoka nchini Algeria yameonyesha ukomavu wa kizalendo ambao umejengeka miongoni mwa wachezaji wa klabu ya Leicester City, ambao kwa sasa wanatolewa macho kila kona ya dunia.

Amesema imekua vizuri kwa mchezaji mwenyewe kusema, hasa baada ya kuzungumzwa kwa kipindi kirefu ambapo kila kiongozi wa klabu iliyoonyesha nia ya kumtaka kiungo huyo alisema la kwake.

Hata hivyo kiongozi huyo amedai kwamba, kauli iliyowahi kutolewa na wakala wa Mahrez (Kamel Bengougam) ya kudai mchezaji huyo ana asilimia “50-50” wanaendelea kuiheshimu na katu hawatoipinga.

Srivaddhanaprabha, amedai kwamba klabu kama Leicester City, haiwezi kupingana na wakala wa mchezaji, na amewataka mashabiki wa soka duniani kutambua kwamba wao hawana sera ya kuuza wachezaji kama ilivyo klabu zingine, lakini ikitokea Mahrez anataka kuondoka kwa bei nzuri hawatokua na hiyana, zaidi ya kumruhusu.

Uongozi Wa Simba SC Washinikizwa Kujiuzulu
Michel Platini Akubali Kuachia Ngazi UEFA