Mashabiki wa klabu ya Simba SC wameandamana na kuvamia makao makuu ya klabu eneo la Msimbazi mapema leo asubuhi kuushinikiza uongozi uachie ngazi kwa madai kwamba wameshindwa kuisimamia timu yao.

Mashabiki hao wenye hasira wameamua kukusanyika kufuatia matokeo ya kufungwa katika na timu ya Mwadui FC katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa jana katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, na kuiacha Simba katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wakitanguliwa na Azam FC walioshinda jana kwenye mechi yao dhidi ya Kagera Sugar.

Jambo lingine lililowapandisha hasira mashabiki hao ni kauli kali aliyoitoa kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kiwelo Julio ambaye amewahi kucheza kwenye klabu hiyo miaka ya nyuma na pia kuwa kocha msaidizi kabla ya kutimuliwa yeye na mwenzake Abdallah Kibaden.

mashabiki-1Baadhi ya mashabiki waliokua wamejikusanya makao makuu ya klabu ya Simba mtaa wa msimbazi jijini Dar es salaam.

Julio alisikika akisema kuwa kitendo cha Simba kufanya vibaya ni laana yake yeye na Kibaden ambao walifukuzwa Simba kihuni na kuletwa kocha Mzungu ambaye hata hivyo naye alifukuzwa baada ya kushindwa kuonesha kile uongozi ulichokuwa unakitaka.

‘Simba ni kama muembe wangu wa uani najiokotea tu dodo ninavyotaka, na siku zote nasema hii ni laana kwa sababu haiwezekani sisi tufukuzwe bila sababu ya msingi halafu aletwe kocha mwingine eti kwa kuwa ni mzungu na cha kushangaza sisi tuliiacha Simba ikiwa katika nafasi ya tatu huyo mzungu wao amemaliza ligi Simba ikiwa katika nafasi ya nne, sasa nani bora? Alisema Julio.

Julio amesema kitendo cha kufukuzwa bila kufuata taratibu za makubaliano kimewauama na kitaendelea kuwauma lakini wamemuachia mwenyezi mungu na ndiyo maana laana inawarudia wenyewe.

Wanaopost picha za watoto wao Facebook, Instagram kushtakiwa
Uongozi Wa Leicester City Wakunwa Na Maamuzi Ya Riyad Mahrez