Hakimu Wilbroad Mashauri anaesikiliza kesi ya kutakatisha fedha inayomkabili aliyekua Rais wa TFF Jamal Malinzi na katibu wake Mwesigwa Celestine ameipa siku 14 upande wa mashtaka uwe umekamilisha ushahidi wote ili kesi hiyo ianze kusikilizwa.
Hakimu Wilbroad Mashauri amefikia hatua hiyo baada ya upande wa mashataka kuileza Mahakama kuwa jalada la kesi ya Malinzi bado lipo kwa DPP ikiwa ni wiki ya tatu sasa.
Upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa TAKUKURU Leonard Swai ulimueleza Hakimu kuwa jalada la kesi hiyo bado lipo kwa DPP hivyo wanaomba tarehe nyingine.
Upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Rweyongeza Richard umesema ni wiki ya pili sasa kila wakija mahakaman wanaelezwa Luwa shauri lipo kwa DPP.
Rweyongeza pia ameileza Mahakama kuwa hivi sasa anazuiliwa kuonana na watej na pia familia ya Aveva na Mwesigwa zimezuiliwa kuwaona ndugu zao.
Akaongeza kuwa ni vema Mahakama ikatoa idhini ili upande wa mashta ukaaambatana n Upnade  wakajaridhishe nini kinaendelea huko kw DPP
Kufuatia hali upande wa uteteza ukaomba uihirisho fupi la wiki moja. Upande wa mashtaka ukaomba aghirisho la wiki mbili ambapo Hakimu Wilbroad Mashauri akakubali ombi hilo la wiki kwa sharti kuwa wakija tena baada ya wiki hizo mbili waje na jibu sahihi ili kesi iannze kusikilizwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Octoba 27 itakapotajwa tena.
Malinzi Mwesigwa na Nsinde Isawale Mwanga wanakabiliwa na makosa mbalimbali ikiwemo kutakatisha fedha makosa ambayo waliyafanywa wakiwa maafisa wa ngazi ya juu ya TFF.‎

Chelsea kumkosa N'Golo Kante wiki tatu
Msemaji wa serikali awataka TUCTA kuacha siasa