Kufuatia azimio lililofikiwa juu ya Mbunge wa Arusha Mjini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema kutakiwa kutohudhuria vikao vya Bunge kwa kipindi cha mwaka mzima yaani kutohudhuria mikutano mitatu ya Bungu kuanzia leo.

Wabunge wa upinzani wameamua kutoka nje ya Bunge baada tu ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka kuwasilisha taarifa hiyo ya kumsimamisha mbunge Lema katika Mikutano mitatu ya Bunge.

Mbunge Lema amefikwa na adhabu hiyo kwa kuunga mkono hoja ya CAG, Mussa Asad ya kudai kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni dhaifu.

Jana Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai aliamuru kamati hiyo kukaa na Mhe. Lema kuthibitisha kauli yake ya kuwa Bunge ni dhaifu.

Sakata hili lilianzishwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ya Serikali CAG, Mussa Assad aliyedai kuwa Bunge ni dhaifu na kauli hiyo ni sahihi kitakwimu kwani inamaanisha upungufu.

Mara baada  CAG kusimamia kauli hiyo Bunge liliazimia kutoshirikiana na CAG jambo ambalo limewaibua watu wengi wakiwemo wanasiasa wastaafu kama vile Pius Msekwa ambaye ni Spika wa Bunge mstaafu ambapo yeye kwa maoni yake amedai kuwa uamuzi wa Spika wa Bunge haujapata kutokea nchini.

Aidha Msekwa ameongezea kuwa uamuzi wa Bunge hautamuathiri CAGA wala Serikali, kwani CAG Assad ana uwezo wa kuondoka nakuja mtu mwingine ambaye ataendelea kufanya kazi kama kawaida.

Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria ajiuzulu
Video: Rais Magufuli akiweka jiwe la msingi kituo cha afya cha Mbonde, Masasi - Mtwara