Michuano ya kombe la mabara inayopigwa nchini Urusi iliendelea hapo jana ambapo ilishuhudiwa mchezo wa kundi A kati ya timu ya Ureno na Mexico ukimalizika kwa suluhu ya mabao 2-2.

Ureno walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia dakika ya 35 kabla ya Mexico kusawazisha kupitia mshambuliaji wao hatari Javier Hernandez ‘Chicharito’ dakika ya 42.

Mchezo huo uliendelea kwa kasi yakushambuliana zamu kwa zamu, ambapo dakika ya 86 mlizi wa Ureno Cedric Soares aliipatia timu yake bao la pili na katika dakika za lalasalama Hector Moreno akaisawazishia Mexico nakufanya mchezo huo kumalizika kwa mabao 2-2.

Video: Nchemba amvaa Lissu makinikia ya Acacia, Hali si shwari mgodi wa North Mara
Nchemba Amtimulia Lissu Vumbi la Mchanga wa Makinikia, Lissu Ajibu

Comments

comments